Kesi za Michael Jackson zafufuliwa upya

Kesi za Michael Jackson zafufuliwa upya

Mahakama kutoka mjini Calfornia wameweka wazi kuzifufua tena kesi za unyanyasaji wa kingono kutoka kwa marehemu Michael Jackson ambazo zilitupiliwa mbali mwaka 2021.

Kwa mujibu wa TMZ inaeleza kuwa uamuzi huo ulifanyika siku ya Ijumaa katika mahakama ya rufaa California ambapo zilifufuliwa kesi mbili kutoka kwa kampuni ya King of Pop's production, mmoja akiwa James Safechuck na Wade Robson wote hao wanamshutumu Jackson kwa kuwazalilisha kwa miaka mingi tangu walivyokuwa watoto.

Inadaiwa kuwa Safechuck na Robson mnamo mwaka 2021 walilishtaki shirika la Michael, MJJ Productions, lakini mashtaka hayo yalitupiliwa mbali, na hii inakuja baada ya hakimu wa Mahakama Kuu ya Los Angeles, ambaye aligundua kuwa kampuni hiyo haikuwa na jukumu la kisheria la kuwalinda wawili hao au mtu mwingine yeyote kutoka kwa MJ kwa sababu haikuwa na uwezo wa kumdhibiti.

Na sasa, mahakama ya juu zaidi inaomba kutofautiana ikimaanisha kwamba kesi za Safechuck na Robson zitarejeshwa kwenye mahakama ya mwanzo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags