Kenya yatoa tahadhari ugonjwa mpya wa zinaa

Kenya yatoa tahadhari ugonjwa mpya wa zinaa

Madaktari kutoka nchini Kenya wamewataka wananchi kuwa waangalifu kufuatia kugunduliwa kwa aina mbili mpya za magonjwa ya zinaa (STIs).

Wanasayansi katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (Kemri) wamepata mabadiliko mawili mapya ambayo wanasema hayajawahi kuonekana katika jeni zinazohusiana na kisonono na klamidia nchini humo.

Ugunduzi huo ulikuja baada ya wachunguzi wakitafuta kuelewa ni kwa nini hospitali mbili katika Kaunti ya Busia, mpakani mwa Uganda, zilikuwa zikirekodi visa vya magonjwa ya zinaa zaidi.

Aidha mtandao wa Kenya wa Nation umeandika kuwa Prof Samson Muuo, msaidizi wa mwanasayansi mkuu wa utafiti katika Kituo cha utafiti wa Mikrobiolojia huko Kemri, alieleza kwamba walishangazwa kuona kwamba wanawake wote 424 wa Kenya walio na umri wa miaka 15 na zaidi waliopimwa kutoka hospitali hizo mbili walipatikana na ugonjwa wa kisonono na klamidia.

Prof Muuo aliendelea kubainisha kwamba mabadiliko ya kisonono na klamidia waliyopata yalikuwa yakishambulia kwa pamoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags