Kariuki aikimbia klabu ya Arsenal

Kariuki aikimbia klabu ya Arsenal

Mwadada Bernice Kariuki kutoka nchini Kenya ambae mpishi wa wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi la klabu ya Arsenal ametangaza kuacha kazi ya kuiandalia chakula klabu ya hiyo, inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL).

Baada ya kufanya nao kazi kwa kipindi cha miaka miwili, mpishi huyo amewashukuru wakenya kwa kumuunga mkono, na kuongeza kuwa

 “Baraka zaidi katika kazi yangu ijayo ni kama ndoto ya kifalme, asanteni sana hasa nchi yangu”alisema Kariuki.

Aidha alijiunga na The Gunners katikati ya mwaka 2021, kama mpishi binafsi wa kikosi cha kwanza, pia alisimamia ustawi wa kila siku na lishe ya timu kabla na baada ya mechi, na chakula cha timu inayosafiri.

Ikumbukwe kuwa Arsenal iliyomaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa EPL, wamekuwa na msimu bora zaidi licha ya kuwa hawaja ambulia kombe lolote msimu huu wa 2020/2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags