Kanye West jukwaa moja na Travis Scott

Kanye West jukwaa moja na Travis Scott

Inasemekana kuwa Mwanamitindo na ‘rapa’ maarufu nchini Marekani amerudi tena jukwaani tangu show yake ya Rants Antisemitic ya mwaka 2022.

TMZ news inaeleza kuwa Kanye West amerejea rasmi kwenye jukwaa, na mtu ambaye amefanikisha kumrudisha Kanye ni Travis Scott.

Kupitia show yake ya kwanza tangu kuachia ‘albamu’ yake ya ‘Utopia’ mjini Roma Traviss aliwashangaza mashabiki baada ya kumpandisha Kanye jukwaani huku akimtambulisha kwa kusema,

“Ni binadamu mmoja tu kwenye sayari hii, ambaye amewahi kutembea nami bega kwa bega kupitia chochote na kila jambo”

Mashabiki walionyesha furaha wakati Kanye akipanda jukwaani, na akiimba "Praise God" wimbo uliomshirikisha Travis kutoka kwenye albamu yake ya "Donda".






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags