Kanye West aomba msaada kwa Kim Kardashian

Kanye West aomba msaada kwa Kim Kardashian

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, #KanyeWest ameomba msaada kwa aliyekuwa mke wake #KimKardashian baada ya kutokuwa na maelewana na kampuni ya Adidas.

Imeripotiwa kuwa msanii huyo amemuomba msaada wa pesa kutoka kwa Ex wake Kim kufuatia mzozo wake na kampuni hiyo iliyozuia mapato ya Kanye kwa sababu ya chuki dhidi ya Wayahudi.

Hata hivyo rapper huyo mwenye umri wa miaka 47 siku za hivi karibuni amejikuta akiwa na hali mbaya ya kiuchumi baada ya baadhi ya brandi nchini humo zikiendelea kumkataa kwa sababu ya mzozo huo.

Oktoba mwaka 2022, Adidas iliacha kufanya kazi na Kanye baada ya kutoa maoni mabaya dhidi ya Wayahudi kwenye mitandao ya kijamii.

Ikumbukwe kuwa Kanye na Kim walifunga ndoa mwaka 2014 na kuachana March 2, mwaka 2022 pia wamebahatika kupata watoto wanne North, Psalm, Saint na Chicago.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags