Kanye West Amrudisha Diddy Mjini

Kanye West Amrudisha Diddy Mjini

Baada ya mwanamuziki na mfanyabiashara Kanye West kumuomba Rais wa Marekani Donald Trump amuachie huru Diddy, sasa amekuja kivingine ambapo ameripotiwa kuingiza sokoni tisheti zenye jina la Diddy.

Kupitia tovuti ya kuuza na kununua nguo ya ‘YEEZY.COM’ tayari kumeweka tisheti ambazo zimeandikwa jina la ‘Sean John’ ikionesha kuwa kwasasa mzigo huo uko sokoni huku akiweka wazi kuwa watagawana wauzo sawa kwa sawa 50/50.

Aidha Ye alifunguka kuwa ushirikianao wa mavazi kati ya chapa yake ya Yeezy na kampuni ya Diddy, Sean John ulipangwa kufanyika kabla ya rapa huyo kukamatwa.


Sean "Diddy" kwa sasa anashikiliwa katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn, New York, akisubiri kesi yake ya mashtaka ya usafirishaji haramu wa binadamu na unyanyasaji wa kingono iliyopangwa kusikilizwa mahakamani kuanzia Mei 5,2025.



Mpaka kufikia sasa Diddy anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono takribani 15, alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16, 2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags