Kanye West akabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji

Kanye West akabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji


Mwanamuziki kutoka Marekani Kanye West anakabiliwa na madai ya kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia aliyekuwa meneja wake aitwaye Murphy Aficionado kwa kumtumia picha za utupu za Kim Kardashian.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo Murphy ambaye alifanya kazi kama meneja wa Kanye mwaka 2022 amemshitaki rapa huyo kwa kumfanyia vitendo visivyofaa wakati wa mikutano ya kazi.

Kulingana na ripoti ya Rolling Stone inaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 2022 kwenye hoteli ya Beverly Hills ambapo Murphy anadai kuwa Kanye alimuita katika chumba ambacho alichokuwa na mke wake Bianca Censori, wakiwa faragha huku akimtaka akae chini na asubiri mpaka alichokuwa akifanya na mke wake.

Aidha mshataki huyo alidai kuwa Kanye na mkewe walikuwa wakifanya tendo la ndoa huku kukiwa na sauti kubwa na kueleza kuwa kitendo hicho kilifanywa kwa dharau na rapa huyo ambapo baada ya kumaliza mambo yake alimfuata Murphy na kumuuliza kama nguo aliyoivaa imempendeza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags