Kanye na Kim Kardashian wakaa meza moja

Kanye na Kim Kardashian wakaa meza moja

Hatimaye #KanyeWest na #KimKardashian wameonekana mgahawani wakipata chakula cha jioni na mtoto wao North, akiwa na marafiki zake ambao walivaa nguo zenye jina la Albamu mpya #Vultures ya ‘rapa’ huyo ambayo imetoka hivi karibu.

Kwa mujibu wa TMZ inaelezwa kuwa pamoja na kuvaa nguo sare lakini pia #Kanye alionekana kujiziba uso wake na mask nyeusi ambayo baadhi ya watu walidai kuwa alivaa kwa ajilii ya kuficha uso wake.

Ni jambo la kushangaza kwa wawili hao ambao waligeuka chui na paka tangu waachane, kuweka tofauti zao pembeni kwa ajili ya kujumuika na binti yao kula chakula cha jioni.

Ikumbukwe kuwa Kanye na Kim walifunga ndoa mwaka 2014 na kupeana talaka mwaka 2022 pia wamebahatika kupata watoto wanne North, Saint, Chicago, na Psalm.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags