Kanye kuchunguzwa na Polisi

Kanye kuchunguzwa na Polisi

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Kanye West ameripotiwa kuchunguzwa na polisi wa LAPD kufuatia tukio lililotokea usiku wa Jumanne baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kumshika kiuno mpenzi wa Kanye, Bianca Censori.

Kwa mujibu wa Tmz inaeleza kuwa Kanye alimpiga na kumjeruhi mwanaume huyo baada ya mtu huyo kumsukuma na kumshika kiuno mke wa Ye, tukio ambalo lilitokea katika bustani za Disneyland.

Hii si mara ya kwanza kwa Ye kujikuta katika uchunguzi wa polisi ikumbukwe kuwa aliwahi kufanyiwa uchunguzi mwaka 2023 baada ya kusambaa kwa video yake ikimuonesha akitupa simu ya paparazi aliyekuwa akimrekodi bila idhini yake.

Hata hivyo kwa mwaka huu Ye ameshitakiwa na mwanaume mmoja ambaye alidai kuwa alipigwa risasi na ‘rapa’ huyo mwaka 2022 kesi inayoendelea kusikiliza katika mahakama ya jiji la Los Angeles.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags