Kanye amtaka Trump kuwatoa jela Larry, Young Thug

Kanye amtaka Trump kuwatoa jela Larry, Young Thug

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Kanye West kupitia podcast aliyoifanya hivi karibuni amesema kuwa hatoweza kumuunga mkono, Rais wa zamani Donald Trump mpaka amtoe gerezani Larry hoover na Young Thug (Jeff) ambaye yuko jela kwa kesi ya kukiuka sheria inayopambana na rushwa (RICO).

Kanye amemtaka Rais huyo wa zamani kumtoa jela Larry na kama itashindikana basi amtoe ‘rapa’ Young Thug (Jeff) jela.

Larry Hoover kwa sasa yuko katika gereza la ADX huko Florence Mjini Colorado, alihukumiwa kwenda jela zaidi ya miaka 150 baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mauaji ya mwaka 1973, utakatishaji wa fedha na uuzaji wa dawa za kulevya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags