Kampuni ya Twitter yafukuza kazi wafanyakazi wote Afrika

Kampuni ya Twitter yafukuza kazi wafanyakazi wote Afrika

Kampuni ya Twitter imewafuta kazi takriban wafanyakazi wake wote nchini Ghana, ikiwa ni wiki moja baada ya bilionea Elon Musk kuchukua uongozi wa kampuni hiyo.

Chanzo kimoja kiliiambia BBC kuwa ni mtu mmoja tu aliyesalia katika timu hiyo yenye takriban watu 20.

Barua za kufukuzwa kazi zilitumwa katika email binafsi za kila mfanyakazi wa ofisi hiyo pekee barani Afrika.

“Huruhusiwi kuwasiliana au kujishughulisha na mteja yoyote, mamlaka, benki au wafanyakazi wengine wa Twitter, na ijulishe kampuni endapo utatafutwa.”

Barua hiyo iliwaambia wafanyakazi kwamba siku yao ya mwisho kazini itakuwa tarehe 4 Desemba, lakini iliwapiga marufuku kutafuta kazi nyingine yoyote kabla ya tarehe hiyo.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags