Kampuni ya Apple yashitakiwa kwa kusababisha mume na mke kuachana

Kampuni ya Apple yashitakiwa kwa kusababisha mume na mke kuachana


Mfanyabiashara wa Uingereza aliyefahamika kwa jina la Richard ameripotiwa kuishitaki kampuni ya simu za Iphone, hii ni baada ya kampuni hiyo kurudisha ‘meseji’ zilizokuwa zimefutika katika simu ya Richard na kusababisha yeye na mkewe kupeana talaka.

Richard ameeleza kuwa baada ya kugombana na mkewe, ndipo mwanamke huyo akachukua simu yake na kuipeleka kwenye moja ya duka la Iphone ambapo mfanayakazi wa duka hilo alimsaidia mwanamke huyo kurudisha ‘meseji’ za mumewe alizokuwa akichati na wanawake wengine.

Hivyo basi mwanamume huyo amedai kuwa jambo hilo lilimsababishia maumivu, uharibifu wa fedha na kupelekea yeye na mkewe kupeana talaka huku akiitaka kampuni hiyo imlipe fidia ya dola milioni 6.37.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags