Kajala: Sijawahi kumfanyia ubaya wowote Anjella

Kajala: Sijawahi kumfanyia ubaya wowote Anjella

Mwigizaji maarufu nchini Kajala amedai alimshauri Harmonize amuachie gari aliyekuwa msanii wa Konde Gang Anjella, alipokuwa akiondoka kwenye Label hiyo,

Kajala amedai kuwa alipoona video ya Anjella kwenye mitandao ikieleza kuwa yeye ndiye chanzo cha Anjella kukosa  support kutoka kwa harmonize alishangaa sana kwani hajawahi kumfanyia ubaya wowote Anjella .

Pia  wakati huohuo Kajala amethibitisha kuwa Harmonize aliwahi kumsaidia baba yake kama alivyodai siku chache zilizopita

Kajala ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akijibu swali la muandishi mmoja juu ya tuhuma za kumfanyia ubaya Anjella.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags