Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema anatazamia kustaafu na kukabidhi madaraka baada ya miaka 23 madarakani.
Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari pamoja na rais wa Kenya, William Ruto katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Kagame alisema mpango wa urithi unajadiliwa kikamilifu na chama tawala.
"Nina uhakika siku moja naweza kujiunga na uandishi wa habari katika uzee wangu na ninatamani hilo liweze kutokea” amesema Kagame
Aidha maoni hayo yamekuja siku chache baada ya chama tawala nchini humo, Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa makamu mwenyekiti.
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Kagame kuzungumzia kuhusu kustaafu, mnamo Desemba 2022, alisema hakuwa na shida kuwa raia mwandamizi wa kawaida.
Chanza BBC
Leave a Reply