Justin Timberlake akamatwa na polisi

Justin Timberlake akamatwa na polisi

Mwigizaji na mwanamuziki wa Marekani Justin Timberlake ameripotiwa kukamatwa na polisi baada ya kukutwa anaendesha gari akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa ABC News, ilieleza kuwa afisa mmoja wa polisi alikiambia chombo hicho kuwa msanii huyo alikamatwa siku ya jana Jumatatu usiku katika bandari ya Sag, New York.

Idara ya polisi jijini humo walithibitisha kuwa aliyekamatwa ni mkali wa Pop, Timberlake huku siku yoyote ndani ya wiki hii atafikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomea mashitaka yanayomkabili.

Hii si mara ya kwanza kwa Timberlake kukutwa amelewa kwani mwaka 2019 picha zake ziliwahi kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii akiwa ameshikwa mkono na mkewe Jessica Beil akiwa amelewa, ambapo siku chaze baadaye mwanamuziki huyo alikili hadharani kufuatia na tabia yake ya ulevi kupindukia.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 anatamba zaidi na ngoma zake kama ‘Better Place’, ‘SexyBack’ ‘Cry Me a River’ huku akionekana katika filamu kama ‘Palmer’, ‘Reptile’, ‘In Time’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags