Julia Fox: Kumiliki Pochi ya Milioni 100 ni Stress

Julia Fox: Kumiliki Pochi ya Milioni 100 ni Stress

Aisee moja kati ya stori ambayo imezua gumzo mitandaoni ni hii inayomuhusu Mwigizaji Julia Fox ambaye anaendelea kuwa maarufu zaidi baada ya kuwa kwenye mahusiano na Kanye West, Julia ameonekana akiwapata Paparazi nafasi ya kumuona na pochi yake mpya ya BIRKIN yenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 100 aliyo zawadiwa na Kanye West kwenye Birthday Yake.

Sasa bwana kutokana na umaarufu huo hivi karibuni Julia alikuwa Paris Ufaransa kwaajili ya kupiga picha za karida la Vogue, Kwenye Interview na New York Times, Julia aliongelea Pochi hiyo nakusema maneno haya.

“Kumiliki pochi ya Birkin na wewe sio tajiri inanipa wasi wasi kila wakati, mara kwa mara naitazama kama bado ipo na haijapotea tuu, ni stress kweli kuwa na hii pochi ya Thamani" alisema Julia.

Ebwana eeeh!! Niambie mdau umewahi kupata zawadi gani yenye thamani kubwa?dondosha comment yako kupitia www.mwananchiscoop.co.tz






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags