Jinsi ya kuzuia unukaji wa miguu, Viatu

Jinsi ya kuzuia unukaji wa miguu, Viatu

Hali ya viatu kutoa harufu mbaya inawezekana iliwahi kukukumba ama bado inakukumba au umewahi kukarahishwa na mtu mwenye tatizo hilo, na kawaida tatizo hilo hufanya mtu kutojiamini, fanya haya ili uondokane na tatizo hilo.

Vaa viatu vinavyokutosha usivae viatu vinavyokubana, kwa sababu unapovaa viatu vya kubana husababisha viatu kutoa jasho jingi ambalo hupelekea ukuaji wa bacteria na fungus wanaotoa harufu mbaya na kuwa kero na wakati mwengine huleta madhara makubwa katika miguu yako.

Vaa viatu ambavyo vinaweza kupitisha hewa mfano viatu vya ngozi au vya wazi ambavyo unajua vitaweza kupitisha hewa.

Badilisha viatu , usivae viatu ‘pea’ moja kila siku hapa usafi unahusika kabisa, ili kuvipa nafasi viatu vingine kama huna fanya usafi wa viatu vyako na soksi kila siku hiyo itaweza kulinda afya ya miguu yako.

Wakati wa usiku au kama kuna kiubaridi usiku viache viatu nje alafu asubuhi vianike kwa kufanya hivyo huweza kuwapunguza bacteria wasababishao harufu mbaya.

Usirudie soksi, hakikisha una soksi za kubadilisha kila siku siyo soksi moja ‘wiki’ nzima, ukifanya hivyo itaweza kukufanya ukapata fungus wa kudumu wanaoweza kusababisha  harufu mbaya kila siku hata

utumie dawa ya aina gani harufu haitatoka kama hautaweza kuzingatia hatua zote hasa kuwa msafi.

Osha miguu yako kila siku kwa sabuni na maji safi yaani hakikisha miguu yako inakuwa misafi muda wote.

Vioshe viatu  angalau mara 1 kwa wiki, uzingatie na malighafi ya viatu husika ili usiviharibu na hata unapoviosha hakikisha vinakauka, epuka kuvaa viatu vikiwa na unyevu .

Vaa soksi pindi unapovaa viatu, hii itasaidia miguu yako kuwa salama maana kuna wakati material ya viatu yakikumbana na joto huleta harufu mbaya.

Tumia majani ya chai kutoa harufu mbaya ya viatu. ‘Pakti’ moja inatosha unaweka kwenye kiatu inaweza kutoa harufu mbaya yote.

Pia kuna ‘Feet up spray’ zinapatikana sehemu mbalimbali maalum kupuliza kwenye viatu vyako ili visitoe harufu mbaya.

Vaa viatu kuendana na hali ya hewa na sehemu unayoenda. Mfano Wakati wa jua kali siyo wakati wa kuvaa viatu vyenye material mazito joto linavutia ‘fungus’ wanaoweza kusababisha harufu mbaya na ya ajabu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags