Jinsi ya kutengeneza juice ya tende

Jinsi ya kutengeneza juice ya tende

Amkeni amkenii kumekucha wajameni, hakuna kulala mama kashasema, kazi iendelee. Sasa wewe endelea kuwa mama wa nyumbani kama ni vizuri, kama kawaida yetu safari hii tumekuja na fursa za kukupatia mawazo mbalimbali ya biashara ambayo hahiitaji mtaji mkubwa sana na ukifanya kwa umakini basi itakufikisha mbali sana.

Kama mnavyojua siku hizi kumekuwa na mvuto mkubwa wa watu mbalimbali kupenda kunywa juisi ya tende, hivyo basi leo tutakuelekeza jinsi ya kutengeneza juisi hiyo ambayo bei yake ni shilling elfu 3,000 mpaka elfu 5,000 kwa glasi moja, sasa unaachaje kufanya biashara hii?

Juisi ina faida nyingi katika mwili wa binadamu. Juisi ya tende ni miongoni mwa juisi zilizojizolea umaarufu mkubwa hasa katika kurekebisha tatizo la nguvu za kiume na kumfanya mwanaume kuwa mwenye kujiamini pale anapokutana na mwenza wake.

Mahitaji yanayotakiwa

  • Tende kilo moja
  • Maziwa ya unga au ya ng’ombe lita moja
  • Sukari kiasi upendacho.
  • Hiriki na tangawizi ya unga

Kumbuka, tende zina asili ya sukari hivyo hakikisha unaweka kiasi kidogo cha sukari ambayo itatosha. 

Jinsi ya kutengeneza

  • Chukua tende zako kisha zitoe mbegu zake.
  • Hakikisha unatoa mbegu tu na kuziacha tende kama zilivyo bila kutoa kitu kingine.
  • Anza kuzisaga pekee yake kwenye blenda hadi zitakapolainika sawasawa. Pia ukiwa unasaga utaweka hiriki yako na ile tangawizi ya unga.
  • Kisha mimina maziwa yako kidogo kidogo kwenye blenda ili kuzisaga vema jambo litakalosaidia juisi yako kulainika vema.
  • Baada ya kutia maziwa yote na kuisaga sawasawa, tia sukari kiasi upendacho huku ukiendelea kuisaga ili sukari yako iweze kuchanganyika vizuri na juisi yako.
  • Halafu chukua chujio na uchuje juisi yako.
  • Hapa sasa juisi yako itakuwa tayari kwa kuuza na kunywa sambamba na kitafunwa chochote ukipendacho kama vile bagia, sambusa, korosho au karanga.

Okay leo haina haja ya kununua vitu vichache kwa ajili ya kujifunza bali hili jambo la leo ni jepesi kabisa kama unavyoona hapo juu, haina kazi sana kama mambo mengine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags