Jinsi ya kupika Pizza ya kuku

Jinsi ya kupika Pizza ya kuku

Uko pouwa wewe? This week kwenye Nipe Dili bhana nakusogezea jambo aadhwimu kabisa, jinsi ya kuandaa na kupika pizza ya kuku nadhani ilikua kiu ya wengi kutaka kufahamu utundu huu basi twende sawa hapa kindakindaki.

Mahitaji:

Nyanya nusu   

Vitunguu maji viwili     

Sereli(kiasi)       

Caroti nne             

Maharage machanga 

Hoho             

Kuku (Steak isiyo na mifupa)         

Tangawizi         

Kitunguu swaum       

Mozzarella Cheese                                     

Jinsi ya kuiandaa

Chukua kuku steak, weka kwenye chombo safi, kisha weka tangawizi kiasi na kitunguu thoum kiasi, chumvi na sereli, maganda ya caroti na maganda ya vitunguu na ndimu kiasi.

Acha kwa muda wa Dk 30, chukua blender, weka kitunguu thoum na tangawizi kiasi pamoja na nyanya na chumvi kidogo na maji kiasi kisha saga vizuri.

Baada ya kusaga, mimina kwenye sufuria kisha pika hadi iwe kama roast nzito.

Halafu, chukua kuku wako steak, weka  kwenye oven hadi awe rangi ya brown (asiungue), hakikisha viungo vinakolea ili kuleta ladha.

Chukua unga wa ngano kiasi weka chumvi kiasi na amira kidogo kisha kanda hadi ulainike.

Tengeneza umbo la duara{weka kwenye oven kabla haujaanza kuumuka). Bake kwa dakika kadhaa kisha ondoa (mkate wa pizza).

Chukua sauce ya nyanya uliyoiandaa sambaza juu mkate (mkate wa pizza) kisha chukua kuku ambaye tayari umemkata katika vipande vidodo vidogo (Steak isiwe na mifupa), weka juu yake kwa kusambaza pande zote.

Kisha chukua maharage machanga yakate vipande vidogovidogo kisha yachemshe kwa dakika chache (hayatakiwi kuiva sana) ni vizuri yakibaki na ukijani wake, yaondoe jikoni halafu chuja maji, kisha chukua maharage sambaza vizuri juu ya pizza. Chukua Mozzarella Cheese kwangua vizuri kisha weka juu ya pizza yako.

Baada ya hatua zote kukamilika rudisha pizza kwenye oven kwa muda wa dakika chache ili cheese iweze kuyeyuka.

Baada ya cheese kuyeyuka vizuri ondoa kisha kata vipande vipande hapo sasa tayari kwa kuliwa.

Siku zote ukifuatilia kipengele cha Nipe Dili lazima utoke na maufundi mapyaa bwana ama nini, komaa na sisi, hakuna kushindwa kitu enjoy your day!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags