Jinsi ya kupika/kutengeneza chocolate cake

Jinsi ya kupika/kutengeneza chocolate cake

Chocolate cake ni biashara ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa ikiwatoa watu kimasomaso kwa kuwabadilishia maisha yao, mwezi Disemba ni mwezi ambao baadhi ya watu hupendelea kupena keki aina ya chocolate so mjanja mwenzangu nimekusogezea dili hili hapa uhangaike nalo na wewe upate pakutokea.

Cake hizi bwana zimeonekana kupendwa siku hizi na watu wa rika zote na bei zake huanzia 5,000 hadi 50k inaweza kufika, na mara nyingi watu hufanya biashara hii kwa kufanya delivery, unaweza kupika nyumbani wewe kazi yako ni ku-post kupitia mitandao yako ya kijamii. cha kuzingatia ni kutengeneza keki zenye ubora ili kuwavutia wateja hata pale uki-post clip au picha wavutiwe.

Mahitaji/vipimo
i. Unga wa ngano vikombe - 2
ii. Sukari vikombe 2
iii. Mafuta kikombe 1/2
iv. Mayai - 2
v. Cocoa robo kikombe
vi. Kahawa ya unga vijiko 2 vya supu
vii. Baking powder kijiko 1 cha chai
viii. Baking soda vijiko 2 vya chai
ix. Maziwa kikombe kimoja na robo
x. Chumvi - 1⁄2 kijiko cha chai

JINSI YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
A) Chukua bakuli weka, ngano , sukari, cocoa, unga wa kahawa , baking powder, baking soda, chumvi vichanganye vyote, kisha chukua mayai yako yaweke pembeni.
B) Kisha chukua maziwa pamoja na mayai yako anza kuchanganya taratibu katika bakuli lako uliloweka unga na vitu vingine mpaka mchanganyiko wako ujichanganye kabisa, angalia usifanye ukawa mwepesi sana.

C) Washa jiko la ‘oveni’ moto uwe 350° - 375° F, kisha paka mafuta kwenye trey yako ya kupikia keki yako.

D) Mimina mchanganyiko wako katika trey ya kupikia keki, pika katika ovener kwa muda wa dakika 35. Epua na subiri ipoe ndiyo uanze kukata vipande.

Ukishaiacha ipoe sasa unatakiwa kutengeneza Sosi ya chocolate au sisi waswahili tunaita rojo ambalo utatumia kumwagia juu kwenye keki yako.
Jinsi ya kutengeneza Sosi ya chocolate
- Chukua suburbia yako weka sukari vikombe viwili au kimoja na nusu.
- Weka cocoa kikombe kimoja katika sufuria yako
- Maziwa kikombe kimoja kisha changanya mchanganyiko wako mpaka uchanganyike wote vizuri kabisa
- Kisha weka sufuria yenye mchanganyiko wako jikoni ukoroge mpaka utakapokuwa tayari kwa sababu ukiachi mchanganyiko wako utaungua.
- Ikishachemka mpaka kubadirika rangi, basi utaweka siagi yako nusu kikombe
- Siagi yako ikishayeyuka na mchanganyiko wako kuwa tayari utashusha jikoni kisha utaweka vanilla vijiko 2, na chumvi kiasi, na utaicha ipoe kabisa
- Kisha utachukua rojo lako na utamwagia kwenye keki yako na tayari kwa kuliwa ama kuuzwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags