Jinsi ya kupika kaimati/kalimati

Jinsi ya kupika kaimati/kalimati

Habari, uko pouwa wewe nikwambie tu leo kwenye Nipe Dili bhana nakuletea jinsi ya kupika Kaimati au Kalimati za sukari,  naamin utaipenda hii ungana name ili uweze kujifunza zaidi.

Tunaze na Mahitaji pamoja na Vipimo vya kaimati hakikisha unazingatia maelekezo ili usije ukaharibu pishi lako.

 

  • Unga - 2 vikombe vya chai
    Hamira - 1 ½ cha chai
    Samli - 1 kijiko cha chai
    Maji - 1 ½ kikombe cha chai (kiasi)
    Mafuta ya kukaangia - kiasi.

Namna ya kutayarisha na kupika.

  • Changanya unga Hamira, Samli, maji, kisha vuruga kulainisha unga hadi uwe hauna madonge na mwepesi kiasi.
  • Funika unga uumuke. Ukiuumuka (ukifura) choma kaimati katika mafuta ya moto.
  • Ziepue na zichuje mafuta.
  • Weka kaimati katika bakuli au sahani kisha mwagia *Shira zikiwa tayari.

Shira

Hapa sasa kwenye kutengeneza shira ya kaimati fuata maelekezo kwa umakini kabisaa usije ukaharibu maana shira ndiyo inayonogesha kaimati.

  • Sukari - 3 vikombe
  • Maji - 1 kikombe
  • Hiliki - ¼ kijiko cha chai
  • Arki (rose flavour) - 3-4 matone

 

Namna ya kutayarisha shira.

 

  • Tia sukari na maji katika kisufuria kidogo, acha kwenye moto ichemke pole pole hadi iwe nzito ya kunata.
  • Tia hiliki na arki ikiwa tayari kumwagiwa juu ya kaimati, huku unavichanganya na huku shira ikipowa na kugeuka kuwa sukari kavu.

 

KIDOKEZO:

Shira ya Kaimati hizi iwe nzito ili unapochanganya na kaimati igeuke kuwa kama sukari ya visheti.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post