Kwenye biashara wiki hii kama kawaida yetu nimekusogozea kitafunwa ambacho wengi wetu hukipendelea kunywa na soda ama juice, ukinywa na chai pia siyo mbaya ila havinogi udugu wangu.
Ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujua dondoo za uandaaji wa kitafunwa hichi.
Mahitaji
- Mayai ya kuchemsha 6
- Viazi vya kuchemsha 12
- Binzari ya unga kijiko 1
- Pili pili manga kijiko 1
- Rangi ya njano ya chakula 1/2 kijiko
- Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
- Tangawizi ilosagwa 1/4 kijiko
- Chumvi kiasi
- Giligilani ya majani (Kotmir) kiasi
- Chenga za mkate kiasi
- Mayai 2 yaliyo chemshwa
- Mafuta ya kukaangia
- Maji ya limao/ndimu 1
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA
- shemsha viazi viive kabisa kisha ponda viazi vizuri kisha changanya pamoja na viungo vyote isipokuwa chenga za mkate na mayai yaliyochemshwa , weka pembeni.
- Chota mchanganyiko wa viazi katika kiganja chako binya iwe flat kidogo kisha tia yai lako na zungusha vizuri kufanya oval shep panga katika sahani rudia mpaka umalize zote
- Tia mafuta jikoni yakipata moto chukua chop yako ichovywe kwenye mayai kisha izungushe katika chenga za mkate na kisha tia kwenye mafuta.
- Kaanga hadi zipate rangi ya brown kisha epua na weka kwenye sahani. Lakini usikaange nyingi kwa mkupuo, fanya hivyo mpaka utakapo maliza zote.
- Kata egg chop yako nusu kisha tia katika sahani yako uloandaa. Egg chop tayari kwa kuliwa na kuuzwa.
Leave a Reply