Aloooooooooh! Kama tunavyo jua sasa hivi wanafunzi wengi wako katika mafunzo kwa vitendo, sasa hapa tumekuja na mada ambayo itakufanya upate maksi nzuri katika field yako.
Mara nyingi field huwa na credit kubwa sana, yani kubwa mpaka inaweza kukusaidia kukubadilishia na kukuongezea GPA yako, Mbali na kuwa unapata mafunzo ambayo yanaweza kukusaidia baadae, na kuwa field ndio sehemu zako za kwanza za kazi ambazo utaziweka kwenye CV yako.
Kupata A kwenye field kunakusaidia sana kwenye matokeo yako ya mwisho lakini pia kuacha mahusiano mazuri na sehemu uliyofanya field ni muhimu kwani hauwezi jua unaweza ukapata reference au sehemu ya internship ukimaliza chuo.
Njia za kupata A kwenye field yako
- Usidoji au kutega field, ukiamua kudoji mtaarifu anayekusimamia field maana atakuja kukusainia kazi uliyofanya, Lakini pia hakikisha unawahi na kufika mapema ili kukabiliana na majukumu yako
- Andika ripoti kila wikiendi, ili usisahau yale uliyoyafanya kila wiki na pia unakuwa unaandika taratibu sio kwa presha kama ukitaka kuzima moto mwisho wa field au supervisor anapokaribia kuja
- Hakikisha siku ambayo masupervisor wanakuja haukosi kuwepo, ukikosa halafu watu wakakupigia simu itakuwa sio nzuri kwa upande wako.
- Jitahidi kufanya kazi unazopewa kwa lengo la kujifunza kwa uwezo wako wote ili pia uonekane unachofanya, Jitoe na uwe unamaliza kazi zako mapema.
- Jitahidi kuwa na mahusiano mazuri na wafanyakazi wengine, Japokuwa ni kwa muda mfupi ila wewe pia ni sehemu ya ofisi, jishushe ili ujifunze.
Jifunze kwa kila mtu Usifike ukawadharau wafanya usafi au technicians kwa vile wewe unasomea kozi ambayo inaweza kukufanya wewe bosi wao, jishushe, kula wanapokula, sikiliza stori zao, mafundisho yao, utajifunza mengi kuhusu kozi, kazi na maisha
- Fanya kazi inayoonekana ili yule anayesaini ripoti yako pale field akusainie vizuri, huo ndio wepesi wa kupata A, usifanye kazi ilimladi umefanya tu kuwa makini na kazi unayoifanya.
- Lakini pia daftari la ripoti lijaze kwa ustadi, pangilia notes vizuri, sio chajuu kinakuwa chini cha chini kinakuwa juu hapana anza mwanzo kati na mwisho.
- Shirikiana na wanafunzi wenzio hata wavyuo vingine. Unaweza pata marafiki wapya lakini pia unaweza pata notes za kujazia kwenye daftari lako la field
- Usichelewe kuanza field, na usimalize pale tu utakaposainiwa na supervisor, fanya muda wote uliopangiwa na chuo. Ukionyesha ustadi mzuri pia sehemu unahofanya field wataona kazi yako, lakini pia wewe utajifunza mengi kuhusu kozi unayosoma.
Ni rahisi sana kupata A field, ila jambo likiwa rahisi ndio huwa tunalidharau na kuhisi tunaweza kulipata kiurahisi bila kujituma pia jitahidi sana kujitoa na kupenda unachokifanya itakusaidia kupata maksi nzuri katika field yako.
Leave a Reply