Jinsi ya kuondoa wasiwasi katika usaili

Jinsi ya kuondoa wasiwasi katika usaili

Heloow! Wanangu wa Mwananchi Scoop, leo nimekuja na kitu ambacho kitakusaidia ili upate kazi kwa haraka. Najua mnadanganyana na kutishana mambo mengi sana kuhusiana na usaili so ungana na mimi ili usipate hofu tena.

Karibu kila mtu hupata wasiwasi wa kiwango fulani kabla na wakati wa usaili. Ni kawaida kuhisi wasiwasi kabla na wakati wa usaili au katika jambo lolote ambalo ni mara yako ya kwanza kulifanya kwasababu unajiona una karibia kuchunguzwa muonekano wako, tabia yako, unachosema na namna unavyosema kabla ya mwajiri kuamua kukupa au kukunyima ajira.

Na siku zote wasiwasi kupitiliza unaweza kuharibu utulivu na ufanisi wako kiasi cha wasaili kusumbuliwa na tabia zinazoweza kuletwa na wasiwasi huo na kushindwa kutilia manani uwezo na sifa zako.

NJIA AMBAZO ZITAKUFANYA KUONDOA HOFU NA WASIWASI KATIKA USAILI

  1. ANZA KWA KUJIANDAE

Maandalizi ni njia bora ya kushinda wasiwasi. Maandalizi yakutosha yatakujengea kujiamini na hivyo kutengeneza nishati chanya kwenye akili yako itakayokufanya ungojee usaili kwa shauku kubwa. Kama jinsi ambayo mwana michezo anavyofanya mazoezi ili awe katika kilele cha ubora wake siku ya shindano. Vivyo hivyo jinsi unavyojiandaa na kufanya mazoezi zaidi, ndivyo utakavyojisikia mwenye kujiamini zaidi.

Maandalizi ya usaili yanahusisha mambo kama kuielewa kazi unayoiomba kujenga uwezo wa kukumbuka uliyoandika kwenye CV yako na kujua namna ya kuyajibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara kwenye usaili.

  1. JIKUBALI

Watu wengi wanachukulia usaili wa kazi kama mahojiano na polisi. Wanahisi hawatakiwi kabisa kufanya kosa kwa hofu ya kuhukumiwa. Ni muhimu kukumbuka kuwa wewe pia unamuhoji mwajiri ili kuona kama majukumu na mazingira ya kazi ni sawa kwako.

Kuufikiria usaili kama mtihani kunaweza kuchochea hisia za wasiwasi na hofu, fikiria usaili kama mazungumzo kati ya watu wawili ambao wanajifunza kuhusu kila mmoja. Hii inaweza kupunguza baadhi ya hisia za shinikizo na kukusaidia kujisikia usiye na hofu kabla na wakati wa usaili.

Hivyo basi kitu cha kuzingatia zaidi ni kujiamini usiangalie mko wa ngapi katika usaili na kusikiliza maneno ya watu kuhusu kushindwa.

  1. KUFIKA MAPEMA SIKU YA USAILI

Jipe muda wa kutosha wa kuelekea kwenye usaili. Toka nyumbani mapema iwezekanavyo ili foleni au hali ya hewa mbaya isikufanye kutofika kwa wakati. Ukishafika, chukua dakika chache kujiandaa.

Kufika kwa wakati ni jambo chanya na waajiri wako watakumbuka, lakini usiingie ndani ya mahali pa usaili zaidi ya dakika ishirini kabla ya muda. Ikiwa unasubiri eneo la mapokezi, zingatia weledi. Wakati mwingine msahili anaweza kumuuliza mtu wa mapokezi kuhusu matendo yako wakati unasubiri.

 

  1. TABASAMU

Hofu husababisha kupumua kwa haraka na huweza kuathiri matamshi na sauti yako. Kabla na wakati wa mahojiano kumbuka kwamba kuvuta pumzi rahisi sana kunaweza kufanya mengi kutuliza hisia za hofu na kupanic.

Kuwa na wasiwasi kwenye usaili ni jambo moja lakini kumuonyesha msaili kwamba una wasiwasi ni jambo linguine Hivyo, kutabasamu kutasaidia angalau kuondokana na sura ya hofu kwenye uso wako, na hivyo wasaili wasiweze kugundua wasiwasi ulionao.

  1. KUJIAMINI

Hata kama hujisikii ujasiri  unaweza kukopa kwa kutumia lugha ya mwili Simama au kaa moja kwa moja, na mabega yako yakiwa nyuma. Hakikisha unatazamana usoni na wasaili wakati wote wa mahojiano, bila kusahau kutabasamu.

Pia, matumizi ya mikono na ishara wakati wa kuzungumza kunaweza kukuonyesha kama mtu unayejiamini. Kumbuka kuwa unapojiweka kama mtu mwenye ujasiri utaanza kujisikia jasiri zaidi kweli. 

  1. JIKITE KWENYE UWEZO WAKO

Usifanye kosa la kuvaa utu wa bandia Fikiria juu ya kila kitu kinachokufanya uwe mfanyakazi mzuri ikiwemo elimu yako, uzoefu wako na sifa binafsi, Kumbuka kwamba mpaka mwajiri anakuita kwenye usaili tayari ameona sifa zako nzuri, hivyo wasaili wananza na hisia nzuri kuhusu wewe.

Fikiria jinsi udhaifu wako unaweza kugeuka kuwa nguvu. Kwa mfano, ikiwa una tabia ya kukubali miradi mingi mara moja, basi unaweza kusema hilo litakuwa na manufaa kama utajifunza kuweka vipaombele na kupanga kazi zako.

  1. ELEWA KUWA KUNAKUPATA NA KUKOSA

Sio jambo la kufurahisha kutopita kwenye usaili, lakini hutokea kwa kila mtu Hivyo usijiadhibu kama usipofanya vizuri. Badala yake, fikiria juu ya kile unachoweza kujifunza kutokana na uzoefu ulioupata na ujitayarishe kwa fursa zitakazofuata. Haijalishi nini kitatokea usaili utakupa uzoefu wa kujifunza ambao utakufanya uwe mgombea wa kazi bora na mkali wa usaili siku za usoni.

Ukiweza kuyafuata hayo mambo basi usahili wako utaweza kwenda vyema kwani utakuwa umejiandaa vya kutosha. All the best!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags