Jinsi ya kuondoa harufu mbaya ya viatu

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya ya viatu

Hellow guys! I hope mko biyeeee kabisaaa, its Friday, mwendo wa fashion kama kawaida yetu bwana. Wiki hii mambo ni moto, mambo ni firee, hatupoi wala hatuboi bwana.

Nikwambie tu wiki hii tutaelekezana jinsi ya kutatua ile changamoto ya harufu inayotoka kwenye miguu pindi ukiwa ushapigilia mchongoko wako bwaana, hahaha make hapo kwanza ncheke, wanangu wa mchongoko hapa tunaelewana bwana.

Basi bwana kama unapitia karaha hiyo usiwaze leo utapata suluhisho kupitia dondoo hii ya fashion karibu.


VIATU KUTOA HARUFU MBAYA 
Hali ya viatu kutoa harufu mbaya inawezekana ilishawahi kukukumba ama bado inakukumba au ushawahi kukarahishwa na mtu mwenye tatizo hilo, leo nitaeleza mambo ya kufanya ili uondokane na tatizo hilo ambalo husababisha watu kutojiamini pindi wanaopokua katika kundi la watu.

 • Vaa viatu vinavyokutosha, usivae viatu vinavyokubana. Unapovaa viatu vya kubana husababisha viatu kutoa jasho jingi ambalo hupelekea ukuaji wa bacteria na fungus wanaotoa harufu.
 • Vaa viatu ambavyo vinaweza kupitisha hewa mfano viatu vya ngozi,nk.
 • Badilisha viatu : Usivae viatu pea moja kila siku. Ili kuvipa nafasi vile vingine. Kama huna vingine, fanya usafi wa viatu vyako na soksi kila siku. 
 • Wakati wa usiku (au kama kuna kiubaridi usiku, viache viatu nje halafu asubuhi vianike) kwa kufanya hivyo huweza kuwapunguza bacteria wasababishao harufu mbaya.
 • . Usirudie soksi. Kufanya hivyo unaita fungus wanaoweza kusababisha harufu mbaya. 
 • Osha miguu yako kila siku kwa sabuni.
 • Vioshe viatu  angalau mara 1 kwa wiki.( Uzingatie na malighafi ya viatu husika ili usiviharibu) 
 • Vaa soksi pindi unapovaa viatu.
 • Tumia majani ya chai kutoa harufu mbaya ya viatu. Paketi moja inatosha unaniacha kwenye kiatu inaweza kutoa harufu mbaya yote. 
 • Pia kuna Feet up spray zinapatikana sehemu mbalimbali maalum kupuliza kwenye viatu vyako ili visitoe harufu mbaya. Harufu inatoka nzuri na utajiamini hasa! Zitumie. 
 • Vaa viatu kuendana na muongo wa hali ya hewa na sehemu unavyokwenda. Mfano wakati wa jua kali sio wakati wa kuvaa viatu vyenye malighafi nzito nzito, joto linavutia fungus wanaoweza kusababisha harufu mbaya na ya ajabu. 

Ebwanaa eeeh mimi nimewakilisha vyema katika kutatua changamoto hii, bila shaka changamkia fursa ili uepukane na fedheha hii, tukutane wiki ijayo. Nice weekiend.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post