jinsi ya kujenga ujasiri wa kukabiliana na changamoto za maisha

jinsi ya kujenga ujasiri wa kukabiliana na changamoto za maisha

Ndugu yangu msomaji hapo ulipo unakabiliwa na changamoto katika maisha na ujui utawezaje kukabiliana nazo?

Je ukikabiliwa na changamoto hizo unatafuta njia za kuweza kuzitatua au wewe ni miongoni mwa wale watu ambao baada ya kujaribu kidogo tu na kushindwa hukubali kushindwa na wala huwa huhangaiki zaidi kutafuta mbinu ya kuzitatua.

Ni ukweli uliyowazi kuwa watu ambao uacha changamoto zishinde wako wengi katika maisha ya sasa, watu hawa hukubali kuwa hawana wanachoweza kufanya na kubaki wamenyongea kwa huzuni.

Tena hata huwa hawafikirii kuitumia fursa hiyo kwa kujifunza maarifa mapya ya kukabiliana na mitihani inayomkabili mtu katika maisha.

Leo inatupasa tutambue kuwa kadri unavyoziacha huzuni ikatuzonga na kuiruhusu zitawale fikra zetu, ndivyo kadri tunavyofanya uwezo wetu wa kuishinda mitihani ya maisha uwe mdogo zaidi.

Hatutaweza kukabiliana na shida na matatizo yanayotufika kwa kuwa wanyonge na wenye majonzi. Kadri huzuni na majonzi yanayoingia katika akili zetu ndivyo kadri uwezo wetu wa kukabiliana na mitihani unavyozidi kuwa mdogo.

 

Inatupasa tufahamu kuwa sisi wote tunapozaliwa huwa ndani yetu kuna mfumo wa neva unaofanya mwili ujihami. Kila tunapokuwa mfumo huu hukomaa na kadri unavyokomaa ndivyo unavyotusaidia kuepuka fadhaa au kuvurugika kwa akili na kutuongezea uwezo wa kuhimili mitihani mbalimbali inayotupata katika maisha.

Changamoto kubwa inayotupata maishani ni uwezo wa kujifunza jinsi ya kuhimili matatizo yanayotupata katika maisha. Lakini tunaweza kujifunza na tutajifunza kutoka wapi? Watu wenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na matatizo ya maisha hawakujifunza shule au chuoni.

Hawa jamani wamejifunza kutokana na uzoefu walioupata katika maisha. Hii ina maana kuwa kadri unavyoishi na kukua na ukapambana na changamoto za aina mbalimbali ndivyo kadri unavyopata uzoefu ambao hauna budi kuutumia kadri uanvyoendelea kuishi.

Watu wenye maisha yasiyo na huzuni au wasiwasi ni wale ambao huwa tayari hata kuthubutu kuchukua hatua za kufanya mambo yenye shaka ili mradi kuvuka changamoto inayotishia kuyafanya maisha yao kuwa magumu.

Basi leo nimekusogezea mbinu ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kukabiliana na changamoto katika maisha yako ya kila siku

Moja unapaswa kujua kwamba kila unapokabiliwa na changamoto ichukulie kama tukio jipya litakalokuwezesha kupima kiwango cha uwezo wako.

Kama kuna jambo unatakiwa kulifanya na hulijui ichukulie hiyo kama nafasi ya kujifunza kutoka popote hata kama kwa watu wengine mradi tu uitatue changamoto hiyo.

Pili, kila unapopata changamoto jiulize kama inaweza kuwa imesababishwa na jambo fulani au inaweza kuwa imetokea tu bila kusababishwa na jambo lolote maalumu.

Baada ya kuitambua sababu itumie kama chanzo cha kuitatua changamoto hiyo. Kwa hakika itakusaidia kuikabili, hata kama haitalimaliza kabisa tatizo hilo itaweza walau kupunguza makali yake.

Tatu inapotokea changamoto ifikirie na ichunguze kwa makini huku ukiilinganisha na changamoto nyingine zilizowahi kukukabili zamani na ambazo uliwahi kuzitatua.

Hapa inakupaswa utafakari vitendo ulivyofanya wakati ule na uone kama unaweza kuvitumia katika changamoto hii. Jiulize ulifanya vizuri kiasi gani? Swali jingine liwe kama ingebidi arudie kutenda alichofanya wakati ule ni mambo gani angeyafanya tofauti na wakati ule?

Nne, Unapopata changamoto inayokukabili jiulize inakuongezea funzo gani katika uzoefu uliokwisha kuupata katika maisha yako. Pamoja na kujifunza wewe binafsi kuna mafunzo gani unayopata kutokana na changamoto hiyo kuhusu familia na jamii inayokuzunguka.

Kutokana na majibu ya maswali tuliyoyatafakari na uzoefu tulionao ni dhahiri kuwa tunapata mwanga na jinsi tunavyoweza kuvuka vikwanzo mbalimbali vinavyotokana na changamoto zinazokukabili katika maisha.

Jambo muhimu zaidi ni kila mmoja wetu kuwa na uwezo wa kuongea na nafsi yake yeye mwenyewe.

Mwish


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post