Na Asha Charles
Hellow!! It’s weekend wafanyakazi kama tunavyojua leo ni siku ya mapumziko, si mbaya ukasoma jarida letu la @Mwananchscoop kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kama tunavyojua wafanyakazi siku zote wanakumbana changamoto mbalimbali kazini kutoka kwa mabosi zao, wafanyakazi wenzao, na hata marafiki zao kazini, so hapa ndo suluhisho lako la kila kitu, tunakushushia mada mbali mbali kuhusu kazi, biahsara, burudani nk…
Hivi kujenga husiano na wafanya kazi au mameneja hapo kazina nalo nijambo gumu jamani? watu wengi maofisini hata sijui kwanini wanakua wagumu kukubaliana na hali ili maisha ya endelee licha ya kuwa wakati mwengine kuna hali ambazo hazivumiliki kwa bosi au meneja katika ofisi.
Unajua siku hizi kila mtu ni mbabe tena ukikuta mtu amekuzidi cheo basi hapo umekwisha sometimes inakuwa nitabia ya kuleta makasiriko kwa wafanya kazi, waswahili wanasema ni hulka ya mtu mwenyewe binafsi.
Kama tunavyojua kunabaadhi ya mabosi wako na hulka ya kuongea sana, kuwa na gubu, kuwazalilisha wafanyakazi wake lakini sasa hivi tumeamua kudilli nao kikamilifu na tabia kama hizi.
Sasa leo nimekuwekea mambo ya msingi ambayo ukiyafanya utaweza kudumisha uhusiano na bosi wako yaani hata awe na gubu kiasi gani na kuifanya kazi yako ivumilie na kujifunza kuishi pamoja.
- Kutana na mwajiri wako/boss
Pendelea kukutana na bosi wako kwa faragha, panga wakati ambapo unaweza kukaa chini nae na kumueleza kila jambo baya analolifanya mfano kuhusu kutokuthaminiwa kazini, kelele na kutamkiwa kauli mbaya anazokutamkia.
Siku zote unaambiwa ni bora kumwambia mtu ukweli hii itakusaidia sana kuliko kuendelea kukaa nalo moyoni litakuumiza kadri siku zinavyozidi kwenda na kukufanya uchukie kazi yako.
Eleza ukweli kwamba bosi wako ndiye anayesababisha shida na hapa unaweza kutumia lugha kama vile "Ninahisi kama sithaminiwi mambo ninayofanya kwa sababu hakuna mtu katika shirika anayetoa taarifa zozote za kuunga mkono." Unapoondoa lawama kwa bosi wako utapata matokeo chanya zaidi. Yaani usiwe mtu walawama itapelekea uonekane hauna adabu sikiliza bosi wako analalamika nini.
Je analalamika kwa kila kitu au kuna mwelekeo wa malalamiko yake? Huenda hayuko salama kuhusu utendakazi wake na hajui kuwa anafanya ubabe.
Lazima utapata jibu kutokana na meeting ulioifanya na bosi wako. Yawezekana kati ya majibu hayo atakuomba msamaha au kujua kama alitaka kumtendea mtu yeyote ubaya kwa mambo yake mwenyewe binafsi pia inaweza kusaidia kuelewa ni wapi bosi wako anatoka kabla ya kukasirishwa na matendo yake.
- Kuboresha utendaji
Fanya kazi kwa bidii na uende zaidi ya wito wa matarajio yako ya kazi. Kuwa wa kwanza kufika ofisini na wa mwisho kuondoka ilimradi kuwe na kazi ya kufanya.
Ukifanya kila uwezalo na kumfanya bosi wako aonekane mzuri, yaan hata iweje ukifanya hivyo bosi wako hatakuwa na sababu ya kukufokea.
Unaweza pia kutafuta njia za kujiboresha, Badala ya kuzingatia bosi wako na matendo yake labda kwa kumsema pembeni, tumia wakati kuboresha mtazamo wako mwenyewe unda maelewano ndani ya kampuni na ujitayarishe kuwatia moyo wengine.
Zungumza vyema kuhusu bosi wako kwa wengine na kwa uangalifu udumishe mtazamo wa uchangamfu wakati wote unapokuwa karibu na wasimamizi na wafanyakazi wenzako kisha penda unacho fanya lazima utakuwa na furaha na na kama tunavyojua furaha huambukiza watu wengine.
- Kuwa na mtazamo chanya
Epuka porojo za kazini hata kama unafanya kazi kwa bidii zaidi ikiwa mara kwa mara unashiriki katika drama za bosi wako nakufanya majadiliano ya kikundi kuhusu bosi wako yataleta hali isionzuri na huna cha kufaidika kwa kumsema vibaya bosi wako.
Na kama huwezi kukwepa maneno ya kuzusha dhidi ya bosi wako au porojo, omba kuhamishwa hadi idara nyingine au ikiwa kazi yako inaathiri mtazamo wako juu ya kazi yako, inaweza kuwa wakati sahihi wakutafuta kazi sehemu nyengine.
Leave a Reply