Jinsi ya kuimarisha afya yako ya akili chuoni

Jinsi ya kuimarisha afya yako ya akili chuoni

Na Magreth Bavuma

Niaje, niaje wanangu kama ilivyo kawaida yetu kupoa ndio kitu tulikataa, karibu tena kwenye segment yako pendwa kabisa ya unicorner sehemu moja tu ambayo tunakuletea story mbalimbali zinazohusu maisha ya wanavyuo na vyuo vyao lengo ni kujifunza na kuelimishana kwa pamoja.

Inawezekana ikawa mara yako ya kwanza kuskia neno ‘Afya ya akili’ au umekua ukiliskia lakini ki aina aina ukawa kama huelewi hivi, tupite kidogo kwenye maana yake ili twende sambamba, kwa maana rahisi kabisa Afya ya akili ni jinsi tunavyojisikia na tunavyofikiri na kuhisi vizuri ndani ya nafsi na kuwa na mawazo mazuri.

Yaani kuwa na furaha, kuwa na ujasiri, na kushughulikia vizuri mambo yanayotufanya tuwe na hofu, wasiwasi au kusumbuliwa na kujenga uhusiano mzuri na watu wengine na kufurahia maisha.

Kwa ufupi, afya ya akili ni kuhisi vizuri katika akili yetu na kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kila siku.

Wanavyuo wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kupoteza au kukosa afya ya akili katika safari yao ya elimu kutokana na kupambana na stress za masomo, na presha ya maisha kwa ujumla  kunaweza kuwa vita halisi kwa akili zao.

Na kwa bahati mbaya baadhi yao hushindwa kutambua kuwa kuzipa nafasi stress za masomo au maisha kunaweza kusababisha wao kuwa na tatizo la afya ya akili ambayo ndio  chanzo cha kupoteza uwezo wa kufanya shughuli zao kwa ufanisi, sasa lazima kuishinda hofu ili  kufanikiwa kuilinda afya yako ya akili na kuna mbinu nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia kujenga afya ya akili na kuendelea kufurahia maisha yao wakiwa vyuoni. Ambazo ni…

  • Kutokuzipa nafasi presha za masomo

Kama mwanafunzi wa chuo kikuu, inaweza kuwa vigumu kuepuka shinikizo la kufanya vizuri kitaaluma hata hivyo haimaanishi kwamba stress za kutamani kufanya vizuri kuchukua nafasi kubwa kiasi cha kupoteza furaha ya kuwa chuoni,  kufanya mazoezi ya kutuliza akili, kupata muda wa kutembelea maeneo kama beach.

  • Kuinjoi (enjoy)

Kuogelea kusikiliza muziki  na mambo mengine yanayoendana na hayo kunaweza kuwa njia bora ya kupunguza stress za masomo. Endelea kufuatilia ratiba yako vizuri na uwe na muda wa kutosha wa kupumzika na kujipatia burudani. Kumbuka, afya ya akili ni muhimu kama ile ya mwili wako.

  • Kujijali

Kujikubali na kujipenda, wakati mwingine tunaweza kuwa wakali sana kwetu wenyewe (being unfair to ourselves) na kujiwekea matarajio makubwa ambayo tunashindwa kuyafikia hivyo kujiongezea msongo wa mawazo.

Lakini ukweli ni kwamba sisi ni binadamu na hatuna budi kukubali udhaifu wetu. Kujijali, kujikubali na kujipenda ndio chanzo cha kuwa na afya ya akili bora. Jifunze kujithamini na kukubali makosa yako kuwa na uhakika na uwezo wako na uamini kuwa unaweza kufanya chochote unachokusudia kwa wakati sahihi.

  • Kutengeneza marafiki wa faida (having the right circle of friends)

Wakati ukiwa chuoni marafiki wanaweza kuwa ndio watu unaowategemea katika mambo mengi hivyo kujenga uhusiano mzuri na marafiki wenye nia njema ni muhimu sana katika kudumisha afya ya akili, panga muda wa kushiriki na kuwa karibu na marafiki zako.

Watembelee pateni muda wa kuongea jifunzeni kuambiana ukweli, na ushiriki katika shughuli za kijamii. Kumbuka, kushiriki furaha na huzuni yako na wengine kunaweza kupunguza mzigo wa hisia zako na kukufanya uhisi kuungwa mkono, kuthaminiwa na kupendwa.

  • Kujenga Muda wa Kujitafakari (You time)

Katika ulimwengu wenye harakati nyingi, tunaweza kupoteza mawazo yetu kugawa vipaumbele vyetu na kuishia kufanya mambo kwa kubahatisha, kujitenga na kelele za dunia na kujitafakari kunaweza kuwa nguvu ya kuboresha na kuimarisha afya ya akili.

Tenga muda wa kuwa pekeako kujipongeza, kujisifia, kujipa nafasi nyingine pale ambapo hukufanya ulivotamani, pia jaribu kufanya mazoezi ya kumediteti (meditation) au yoga, fanya safari fupi za ki pekee yaani peke yako au tumia diary yako kuandika mambo yanayoupa furaha moyo ( siku hizi wanaita kumwagilia moyo ) wako ukiwa peke yako.

Kupata muda wa kujitafakari kunakuruhusu kujikumbusha thamani yako na kuwa na mtazamo mzuri katika maisha yako.

  • Kuomba msaada wa kitaalamu

Kama vile mwili wako unapoweza kuugua na kuhitaji matibabu, hivyo ndivyo akili yako inaweza kuhitaji msaada wa ziada. Usiogope kuomba msaada wa kitaalamu ikiwa unahisi kuwa hali yako ya kiafya ya akili inakuzidi.

Kwa kawaida vyuoni huwa kunakua na huduma za ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi, tafuta msaada huo na usiogope kuwasiliana na wataalamu wanaostahil weka aibu pembeni katika kutafuta msaada na inaweza kuyabadilisha maisha yako ukiwa chuoni kwa sehemu kubwa.

Kumbuka, wewe ni shujaa wa hadithi yako mwenyewe, wakati wa safari yako ya elimu, afya ya akili inapaswa kuwa kipaumbele chako. Hakikisha unakua na furaha na uyakubali na kuyafurahia maisha yako,  ukifanikiwa katika hilo utakuwa umeweza na maisha yako wakati ukiwa chuoni yatakuwa bomba na ukajikuta unakua mfano wa kuigwa na wenzio wote wakatamani kujua siri ya furaha na mafanikio yako.

Haya sasa ni muda wako wa kuipa kipaumbele afya yako ya akili jiambie kila siku mimi ni wa muhimu, i can do this and i come first, tukutane tena wakati mwingine segment ni moja tu unicorner tchaaooooo..






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags