Jinsi ya kufungua akaunti ya Whatsapp iliyofungiwa

Jinsi ya kufungua akaunti ya Whatsapp iliyofungiwa

Kama tunavyojua kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na baadhi wa watu kulalamikia akaunti zao za WhatsApp kufungiwa mara kwa mara bila ya sababu yoyote sasa @Mwananchiscoop tupo hapa kukujuza namna ya kufungua akaunti hiyo.

  • Sajili upya namba yako ya simu kwenye WhatsApp

Hapa uta-download Application ya WhatsApp au WhatsApp Business, kisha anza kujisajili upya namba yako na kufuata taratibu zote, na ikiwa akaunti yako bado imefungiwa unaweza kusubiri kwa siku 30 na ujaribu tena.

  • Tuma ombi la msaada (Help) WhatsApp

Download tena program ya WhatsApp kisha nenda sehemu iliyoandikwa ‘Help’ bonyeza itakupa maelekezo na uyafuate kisha jaza ombi lako na ubonyeze kwenye kitufe cha ‘tuma usaidizi’

  • Tuma Barua pepe kwa WhatsApp

Ingia Google kwenye ukurasa wa mawasiliano wa WhatsApp, kisha nenda sehemu iliyoandikwa ‘Contact WhatsApp’ na italeta maelekezo ya kuchague kama akaunti yako ni ya kawaidia au business kisha utakuta 'fomu' jaza na utume, baada ya dakika tano utapokea email moja kwa moja kutoka WhatsApp na watakufungulia akaunti yako.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post