Je wajua kwanini Messi anaitwa ‘la pulga’

Je wajua kwanini Messi anaitwa ‘la pulga’

Alooooweeee! Alootenaaa! Ila tuache masihara bwana watu wangu wa segment ya burudani nimewamisi mnoo, haya leo bwana tumeshuka na mada ambayo baadhi ya watu watakuwa wanajua lakini mimi nakujuza Zaidi na asiejua aweze kujua.

Katika burudani tumekusogezea mwanasoka mkongwe mwenye mataji mengi zaidi kufuatiwa na jitihada anazozifanya katika kazi yake ya mpira wa miguu.

Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kwanini Messi anaitwa ‘La Pulga’ mashabiki wa mwamba huyo wamekuwa njia panda kwakuwa hawaelewi maana yake, so ungana nami mwanzo mpaka mwisho kwa kujua kujua zaidi.

Wanasoka mashuhuri waliopita wamepokea majina mengi ya utani. Majina ya utani yanategemea zaidi mtindo wao wa kucheza, sifa na tabia. Kwa upande wa mshindi wa kombe la dunia mwaka 2022 Lionel Messi mara nyingi hujulikana kama ‘MBUZI’ na ‘La Pulga kwa baadhi ya mashabiki.

Jina la utani la Lionel Messi ‘La Pulga’ maana yake halisi ni  ‘The Atomic Flea’ kwa Kiingereza, anaitwa ‘The Atomic Flea’ kutokana na umbile lake na uchezaji wake kwakua  ni mwepesi, sana wa kuwapita mabeki kadhaa kwa urahisi na kwenda kufunga.

Tangu utoto wake popote pale alipocheza, amekuwa mchezaji mdogo zaidi uwanjani. Alikuwa na futi 3 na inchi 6 tu alipokuwa na miaka 9. Urefu wake, hata hivyo, ulionekana kuwa faida isiyo ya haki kwake.

Kwakua wenzake wote walikuwa warefu na wakubwa kuliko yeye, lakini hakuna aliyeweza kutikisa mpira miguuni mwake. Mabeki wanamzunguka kutoka kila mahali, lakini kwa namna fulani anafanikiwa kutoka na mpira.

 

Wengi mnasubiria kujua Lionel Messi alipataje jina lake la utani?

Mnamo 2005, Lionel Messi alifunga mabao kadhaa katika uwanja wa Barcelona. Ndipo Mwandishi wa habari wa Argentina alimtaja 'Pulguita' au 'Kiroboto Kidogo' Lakini kaka zake Messi walimwita mdogo wao ‘kiroboto kidogo’ kwa sababu ya kimo chake kidogo na mtindo wa uchezaji wake.

Alianza kufunga mabao zaidi na kusaidia timu yake ya Barcelona kushinda mechi peke yake ‘Kiroboto Mdogo’  haikusikika kuwa ya kubembeleza tena.

Uwezo wake wa kuwabwaga wachezaji na kuweka mikwaju hiyo kwenye kona ya chini ikawa hali ya mara kwa mara, Jina lake la utani lilibadilika na kuwa 'La Pulga' au 'The Atomic Flea' na lilidumu/linadumu mpaka sasa.

Amekuwa akicheza dhidi ya mabeki warefu wa upinzani, ambao walijaribu kumzidi nguvu Lakini uwezo wake na kipawa cha kupita katika nafasi zilizobana kila mara ulimfanya awe bora zaidi.

Mbali na wepesi wake wa kuzaliwa na uwezo wa kufunga mabao, pia ana jicho la ajabu la kupiga pasi. Maono yake yasiyo ya kawaida yanaweza kuchagua njia ambazo siyo ya kawaida kwa macho ya mwanadamu hayawezi kamwe kufikiria.

Hapo awali nilizungumza kuhusiana na ndugu wa mwanasoka huyo so wacha nikupe stori kidogo kuhusiana kaka haoo…

Nyota huyo wa Argentina ana kaka wawili wakubwa mbele yake ambao hawajulikani sana katika mitandao ya kijamii  Rodrigo Messi ndiye kaka mkubwa, Matias na Lionel Mess, Rodrigo Messi yeye ni Mfanyabiashara wa Michezo.

Matias Messi ana Zaidi ya  miaka 40 na ni mtu mwenye utata. Matias amekuwa akikabiliwa na mashtaka kadhaa ya kisheria kwa miaka mingi. Ameshtakiwa kwa kubeba silaha isiyo na kibali na kuwashambulia maafisa wa polisi.

Haya haya yaani leo nimejifunza jambo kubwa sana, sio kila jina la utani unalopewa linamaanisha ubaya tuu kuna baadhi yao yanamaanisha vitu ambavyo uko navyo ndani yako so usichukie kwa majina ya utani unayopewa huwezi jua aliekuita hivyo ameona maano gani kutoka kwako ilimladi tu lisiwe baya.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post