JayMelody: Nampenda Paula

JayMelody: Nampenda Paula

Alooh huku ni kutangaza vita na P Funk Majani kabisaa hahaha Hit Maker wa Sugar Jay Melody Amefunguka juu ya Hisia zake kwa Paula Kajala.

Ebwana hii imekuja baada ya kumpost Mrembo huyo kwenye Ukurasa wake wa Instagram na Kuifuta baada ya Muda mfupi tu .

Akiwa kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari  ametolea Ufafanuzi mpaka kupost picha ya Mrembo huyo na badae kuifuta Amesema...

"Mimi Paula Nampenda kama watu wengine ninavyowapenda naziona picha zake nzuri ndio maana nikaamua kumpost lakini nilichokiandika havihusiani na picha yake ndio maana nilitanguliza picha yangu. Hakuna ubaya katika hilo.

"Hakuna mtu yoyote alienicheki lakini picha niliifuta baada ya kuona Coment zimekuwa Nyingi hadi wajomba zake nikaona sina haja ya kumtengenezea mtoto wa watu Mawazo nikaona ni bora niifute".


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post