Rapa Jay Z na familia yake wanaripotiwa kupokea vitisho vya kuuawa kutokana na kesi ya ubakaji kwa binti wa miaka 13 anayodaiwa kufanya akiwa na Diddy mwaka 2000.
Jay anadai amekuwa akipokea vitisho yeye na familia yake kutoka kwa watu mbalimbali mitandaoni wakiwatuhumu kuwa ni waongo, waovu huku wengine wakitaka rapa huyo aswekwe gerezani kama Diddy na kisha auliwe kabisa.
Aidha kesi hiyo ambayo imekuwa ikizua mijadara mingi mitandaoni tayari imeshafutiliwa mbali baada ya aliyefungua kesi hiyo kwenda kuifuta mahakamani kwa hiyari.
Utakumbuka Jay na Diddy walifunguliwa mashitaka na mwanadada aliyefahamika kwa jina bandia la 'Jane Doe' Desemba 9, 2024 akidai kuwa nguli hao katika rap walimbaka mwaka 2000 baada ya sherehe za tuzo za Video Music Awards VMAs.

Leave a Reply