Jay Mondy aweka rekodi postiwa na YouTube

Jay Mondy aweka rekodi postiwa na YouTube

Baada ya kusota kwa miaka mingi katika uchekeshaji, sasa tunaweza kusema mchekeshaji na dansa  maarufu nchini Tanzania Jay Mondy amejipata. Hii ni baada ya kupostiwa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa YouTube kwa kuwa miongoni mwa dance waliofanya  vizuri kwenye chalenji ya wimbo wa Tyla uitwao Art.

Jay anakuwa dansa pekee kutoka Afrika Mashariki kupostiwa na YouTube ambapo mtandao huo uliamua kufanya hivyo kwa watengeneza maudhui mbalimbali ambao wanaupiga mwingi  mmoja wapo akiwa Jay.

YouTube imetoa orodha hiyo ikiwapongeza watengeneza maudhui kutoka mataifa mbalimbali kufuatia na juhudi wanazozifanya pamoja na maudhui yao kufanya vizurri.

Kwa sasa Jay anazunguka mataifa mbalimbali akiwa na mpenzi wake Isabella Afro ambaye pia ni dansa aliyejulikana zaidi kupitia baadhi ya video za mwanamuziki Diamond, ambapo katika mataifa hayo Jay amekuwa akitumia fursa ya kufanya challenge za kucheza nyimbo ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika mtandao huo wa YouTube.

Kupitia heshima hiyo iliyotolewa na YouTube baadhi ya mashabiki wameonekana kuvutiwa na kitendo hicho ambapo wengi wao wamempongeza mchekeshaji huyo kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Jay Mondy alianza sanaa akiwa kama mchekeshaji wa kuposti video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na kusimama katika ‘Starndup Comedy show’, na rasmi alianza kujikita katika dansi mwaka 2020.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags