Jason Momoa athibitisha kutoka kimapenzi na Adria Arjona

Jason Momoa athibitisha kutoka kimapenzi na Adria Arjona

Baada ya kuzuka tetesi kuhusiana na Mwigizaji wa Marekani Jason Momoa na Adria Arjona wanatoka kimapenzi, hatimaye Momoa amethibitisha tetesi hizo.

Momoa amethibitisha kutoka kimapenzi na mwanadada huyo wakati alipoulizwa swali katika kipindi cha ‘Entertainment Tonight’, kuhusiana na mtu gani ambaye anapenda kupanda pikipiki yake ambapo Momoa alieleza kuwa ni mpenzi wake Adria Arjona na huwa anavutiwa sana akimkumbatia wakati wa kuendesha pikipiki hiyo.

Uvumi wa wawili hao kuhusishwa kutoka kimapenzi ulianzia baada ya Momoa ku-share picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa Japan na Arjona wakiwa kwenye penzi zito.

Utakumbuka kuwa Momoa alikamilisha mchakato wake wa talaka na aliyekuwa mkewe Lisa Bonet Januari 2024 ambapo wanandoa hao walioana mwaka 2017 na kutengana 2022 huku wakifanikiwa kupata watoto wawili Nakoa-Wolf (15) na Lola (16).

Aidha Jason Momoa na Adria Arjona walikutana kwa mara ya kwanza katika filamu ya ‘Sweet Girl’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags