Janus paka aliekuwa na sura mbili

Janus paka aliekuwa na sura mbili

Oooooh! Ama kweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, basi bwana hii kitu imezoeleka tuu kuonekana kwa binadamu tu lakini kumbe hadi kwa wanyama, hapa tunazungumzia watu kuzaliwa wakiwa wameungana. Leo bwana nimekusogezea paka ambae ameungana uso.

Frank na Louie au Janus paka mwenye sura mbili Janus paka aliyeishi zaidi duniani (1999 - 2014) kutoka Massachusetts, Marekani walikuwa na nyuso mbili zilizokaribiana, kutokana na hali ya kushangaza sana ya kuzaliwa inayojulikana kama diprosopia.

Paka Janus mara chache huishi zaidi ya siku moja baada ya kuzaliwa kwao. Tangu kuonekana kwake kwa mara ya kwanza kupitia rekodi Guinness World Records mwaka wa 2006, Frank na Louie wamekuwa wakitrend sana kwenye vyombo vya habari, kamavile magazeti na mitandao ya kijamii.

Mmiliki wa paka wao alifahamika kwa jina la Marty ambaealikuwa akifanya kazi ya uuguzi wa mifugo ndipo akampata paka huyo akiwa ameenda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji lakini ilishindikana.

Mhudumu huyo alieleza jinsi alivyokuwa akiwatofautia na kusema kuwa  paka wa upande wa kushoto ni Frank na wa upande wa kulia alitambulika kama Louie

Kama paka, alihitaji utunzaji na uangalifu mwingi muhudumu huyo aliwalisha kila baada ya masaa mawili na fomula maalum ya kulea wanyama kama paka.

Hatimaye Frank na Louie wakawa na nguvu za kutosha kucheza na paka wengine na wakawa marafiki wa pekee na mbwa wa familia. Hata alitolewa nje akiwa na Kamba shingoni kwaajili ya matembezi.

“Kama wavunja rekodi wengine Frank na Louie walikaidi uwezekano na kuingia katika vitabu vya historia kwa hadithi yake ya ajabu  kwa kesi yake, kushinda masuala ya matibabu na kuishi maisha marefu na yenye furaha," alisema Mhariri Mkuu wa rekodi ya Guinness Craig Glenday. wakati huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post