Jamie Foxx kuja kama Celine Dion

Jamie Foxx kuja kama Celine Dion

Mwigizaji wa Marekani Jamie Foxx amedai kuwa yupo tayari kuzungumzia changamoto na mapito aliyoyapitia wakati alipokuwa mahututi.

Foxx anatarajia kuelezea mapito hayo kupitia onesho lake linalotarajia kuanza mwezi ujao lililopewa jina la ‘What Had Happened Was’ ambapo Foxx atasimulia na kuonesha picha pamoja na video kuhusu tatizo lake la kiafya lililoanza wakati wa kurekodi na kusababisha alazwe hospitalini mwaka jana.

Aidha kwa mujibu wa Foxx kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa usiku huo utakuwa na mambo mbalimbali yakiwemo kicheko, maumivu na mahusiano ya karibu ambapo imepangwa kufanyika Oktoba 3, 4, na 5 huku tiketi zikinza kuuzwa hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa Juni 25, 2024 mwanamuziki Celine Dion aliachia filamu ya mapito wakati alipokuwa akisumbuliwa na ugonjwa wake wa ‘Stiff Person Syndrome’ uliomuanza toka mwaka 2008, filamu hiyo iitwayo ‘I Am: Celine Dion’.

Jamie Foxx alikimbizwa hospitalini matatizo ya kiafya Aprili 2023, tatizo hilo lililomuanza wakati wa ku-shoot filamu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags