Jada Smith afichua kutengana na Will kwa miaka saba sasa

Jada Smith afichua kutengana na Will kwa miaka saba sasa

Muigizaji na mtangazaji kutoka nchini Marekani Jada Smith ameweka wazi kuwa yeye na mume wake Will Smith ambaye pia ni muigizaji walitengana kwa siri miaka 7 iliyopita huku akieleza kuwa hawana mpango wa kupeana talaka.

Kufuatia mahojiano yake leo asubuhi na NBC News baada ya kuulizwa kuhusu hali yao ya ndoa alieleza kuwa yeye na mumewe walitengana kwa siri toka mwaka 2016 licha ya kujaribu kurudisha uhusiano wao lakini haikuwezekana.

Jada alifichua kuwa hata wakati wa Tuzo za Oscar 2022, Will alipompiga kibao Chris Rock, walikuwa wametengana kwa miaka sita.

Hata hivyo Jada ameeleza kuwa kwa sasa bado wanaendelea kutafakari kuhusu kutengana kwao kwa sababu wamekuwa wakipeana support huku akiamini kuwa bado wana upendo wa dhati kati yao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags