Irene Uwoya amvaa anayedai amefanya kanisa kama disko

Irene Uwoya amvaa anayedai amefanya kanisa kama disko

Mwigizaji Irene Uwoya amemvaa mama anayehoji kuhusu kuokoka kwake, kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mama huyo akidai kuwa Irene anatakiwa kufundishwa kwanza ndiyo awe mtumishi kwani kanisa siyo disko, imeonekana kumkera mwigizaji huyo hadi kufikia hatua ya kujibu.

Alichosema mama huyo ambaye jina lake halijafahamika.

"Irene Uwoya karibu kwenye Ukristo lakini Ukristo ni gharama kaa ufundishwe siyo unakurupuka tu juzi unaanza kusema wewe ni mtumishi, mchungaji kwa nini unafanya kanisa kama ukumbi wa disko kila mtu anakuja kucheza mdumange, kama umeokoka kaa ufundishwe una mambo mengi umemtumikia adui muda mrefu unatakiwa uoshwe uondolewe kila aina ya takataka ufae, siyo leo unakuja kutamka wewe ni mchungaji kwa sababu ni maarufu huku siyo kwenye siasa,"amesema.

Hata hivyo, kutokana na kauli hiyo Irene kupitia ukurasa wake wa Instagram amedai kuwa anachokifanya hajataka yeye bali Mungu kamuita.

"Biblia imeandika watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, naomba kumuuliza huyu mama lini amewahi kuja kanisani kwangu? nani alimwambia nina kanisa? nani alimwambia mimi mchungaji? kuna watu wanapenda sana kukwaza watu yaani mtu uongee ujikute umemtukana mtu iwe shida nilisema sitaongea ila acha niseme. Naomba anayemjua huyu mama amwambie akaangalie YouTube yangu nimeongea kila kitu.

"Pia mwambieni Mungu ndiyo ameniita sijajiita, pia ajue kwamba hii njia nilipo siyo rahisi naomba asiniongezee ugumu nikamkosea Mungu pia mimi ni Mkatoliki tangu nazaliwa ila namtumikia Mungu jinsi alivyoniagiza nafuata maelekezo ya Mungu na siyo binadamu aache kuropoka vitu hajui kama mwehu sababu anaonekana amechanganyikiwa," ameandika Irine.

Hata hivyo, amemtaka aache kumzungumzia ili baadaye ashuhudie ukuu wa Mungu.
"Naomba sana achunge mdomo wake maana sisi wengine tukilia kwa Mungu ni tatizo na mimi namhitaji bado aje ashuhudie ukuu wa Mungu ndani yangu," ameeleza Irene.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags