Illbliss: Burna Boy, Davido na Wizkid ni Ma-Rapa

Illbliss: Burna Boy, Davido na Wizkid ni Ma-Rapa


‘Rapa’ na mwigizaji Tobechukwu Ejiofor, maarufu kama Illbliss, amezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba Burna Boy, Davido, na Wizkid ni ma-rapa.

Illbliss ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye moja ya mahojiano, yake ya hivi karibuni akielezea namna muziki Afrobeat ulivyowaondoa ma-rapa wa zamani ambao ni top three ya wasanii wakubwa Nigeria.

“Tulipoteza askari wetu wengi; tulipoteza Burna Boy, Wizkid, na Davido. Watatu hao walikuwa ma-rapa," alisema rapa huyo.

Aidha aliongezea kwa kudai kuwa Burna Boy, Wizkid, na Davido washukuru sana muziki wa Afrobeat kwani wangeendelea na muziki wa ‘rap’ basi wasingeweza kupita mafanikio yake.

Illbliss anatamba na ngoma zake kama ‘Chukwu Agozigo Gi’, ‘Bizness’, ‘Kiss The Ring’ na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags