Ijue zaidi biashara ya nguo za mitumba

Ijue zaidi biashara ya nguo za mitumba

Hello! Mambo vipi pande hizo, swaumu inapanda au niwaache kidogo? Kama tunavyojua bwana ni mwezi wa ramadhani na unatujulisha kuwa Eid iko karibuni, so biashara ambayo itakufanya utoboe kipindi hichi ni uuzaji wa nguo.

Bwana huu sio uongo, sisi wabongo huwa tunapenda sana na tunazikubali nguo za mitumba, yaani mkubali mkatae, ndo nguo watu wengi wanazozikubali kusema ukweli.

Sasa leo tumekuja na wazo la biashara ya kuuza nguo za mitumba, na nimekumbuka kitu kumbe mbele hapo kuna sikukuu ya pasaka bwana biashara zipo ni sisi tuu kuamua kuzifanya.

Kama tunavyojua watanzania wengi hupendelea sana kuvaa nguo za mitumba ni kwasababu kwanza ndo uwezo wetu ulipo kila mmoja anaweza kuaford kusema ukweli, pili ni ubora na uimara wa nguo hizo kila mtu anazijua hazichakai haraka.

Tuseme tu ukweli mavazi ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya binadamu, kwasasa biashara inayokua zaidi ni ya mitumba na ina faida kubwa sana kutokana na aina ya nguo.

Kwa mfano ukinunua balo grade one moja  lina faida mara mbili na thamani uliyonunulia na sio kila mtumba zinalipa bali uchaguzi wa nguo nzuri.

Wacha leo niwaibie siri ya watu wanaofanya hii biashara, mabalo ya nguo mengi huanza kuanzia 380,000 mpaka 480,000 au 520,000 inategemea na ulipo na mzigo unabeba pisi 100 hadi 250 kwa balo moja.

Naona nishaanza kuwasanaua baadhi ya watu hapa yaani hii biashara ndani yam waka tajiri wewe mjini, kwa kuanzia mtaji uwe tu na hiyo 500,000 ili uweze pata balo moja kama kawaida yetu sio lazima uwe na duka ndugu yangu uzia hata chumbani na mambo yataenda hiovyo hivyo kwa kuforce cha muhimu ni kutangaza nguo katika mitandao ya kijamii.

Mabalo ya kiume mara nyingi huwa yana anzia 350k na kuendelea, ila kwa kukushauri huko ulipo kama unataka kununua nenda na mtu ambaye anajua hiyo biashara ili akuchagulie belo zuri, coz kuna lebal za kuchukua sio kila mzigo unachuka zingatia hilo wanaweza kusema wamekupa namba moja kumbe sio.

Ushauri wa bure kabisa kwanzaa angalia kama eneo lako kuna hali gan ya hewaa kama ni baridi kachukue "shifoni" ni 180000

Chimbo ambalo watu wengu hununua mabalo au wanako uza balo ni pale mnazi mmojaa mtaa wa sofiaa sasa usikurupuke tuu kwenda kununua inabidi ufanye survey kabla ya yote si unajua bongo hii unaweza ukapigwa na kitu kizito.

kama tunavyojua siku zote biashara hazitaki hasira wala haraka unaweza ukaanza kidogo kidogo kama tuanvyojua siku zote biashara inaitaji subra mnoo.

Kwenye kuuza nguo hapa kwa mfano mashati grade one-two ya mtumba jijini dar-es-salaam ni shilingi 3000 na mikoani shati hilo hilo shilingi 7000. So uchaguzi ni wako kuuza hapahapa Dar au mkoani lakin ukumbuke tuu mkoani kuna pesa ya usafirishaji.

Biashara hii inatoa fursa kwako kuanza na mtaji mdogo na kuendelea uchaguzi ni wako kuanza na mtaji mdogo au mkubwa

Nyieee nyieee huu ni mwaka wetu lazma tutoboe hakuna kukaa kizembe wakati fursa zipo nyingi ni kuchukua tuu hatua ya kuacha kuwa beki tatu, I hope mmejifunza vitu vingi usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii @Mwananchiscoop ili uweze kujifunza mambo kadha wa kadha






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags