Idadi ya watu waliouwawa kwa kunyongwa yafikia 883,Duniani

Idadi ya watu waliouwawa kwa kunyongwa yafikia 883,Duniani

Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema katika ripoti yake kuwa idadi ya watu waliouawa kwa kunyongwa ulimwenguni kote mwaka uliopita, imeongezeka kwa asilimia 53.

Amnesty imesema idadi hiyo imefikia watu 883, hiyo ni idadi ya juu zaidi ya matukio hayo tangu mwaka 2017.

Sambamba na ripoti ya shirika hilo imeyashutumu hasa mataifa ya mashariki ya kati na kaskazini mwa Afrika, ikiwa ni pamoja na Iran, Saudi Arabia na Misri, ambayo yanafahamika kwa kutekeleza adhabu ya ya kunyonga.

Ripoti hiyo imebaini kuwa usiri wa serikali za Korea Kaskazini na Vietnam pamoja na upatikanaji duni wa taarifa katika nchi kadhaa, vinazuia utoaji wa tathmini kamili ya hukumu ya vifo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags