Imekuwa kawaida kwa watumiaji wa iPhone kuhitaji baadhi ya usaidizi kutoka kwa Siri, kama vile kumuuliza maswali. Hivyo basi kutana na Susan Bennett, ambaye ndiye mwenye sauti ya Siri.
Susan Alice Bennett ni mwigizaji wa sauti na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Sauti yake ndiyo hutumika kama Siri wa Apple, tangu huduma hiyo ilipoanzishwa kwenye iPhone 4S Oktoba 4, 2011 hadi toleo la iOS 7 mwaka 2013.
Mwanamama huyu hajaishia tu kwa Siri pia hujipatia pesa kupitia matangazo ya biashara, mifumo ya GPS na kuhutubia wasafiri katika vituo vya ndege vya Delta.
Katika mahojiano aliyowahi kufanya na CNN Business alieleza kuwa safari yake ilianza mwaka 2005 wakati ScanSoft kampuni ya programu za simu, ilipokuwa inatafuta sauti kwa ajili mradi wao mpya.
Hata hivyo, wakati huo alikuwa tayari amefanya kazi nyingi na GM Voices, ambayo ni kampuni na kituo cha kurekodi ambacho kinajishughulisha na vidokezo vya sauti zinazotumiwa kwenye programu za simu.
Hivyo sauti yake ilichaguliwa na ScanSoft, Juni 2005 Bennett alitia saini mkataba wa kutoa sauti yake. Alidhani ingetumika katika mifumo ya simu za kampuni hakujua kama ingeweza kuwafikiwa watu wengi duniani.
Oktoba 2011, baada ya Apple kutoa iPhone 4S ya kwanza kuwa na Siri. Bennett hakuwa na simu, lakini watu wa karibu waliokuwa na simu hiyo waliifahamu sauti yake wakamtafuta na kumueleza kuwa kwenye Iphone mpya inatumia sauti yake. Susan alizaliwa Julai 31, 1949.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply