Mwanamuziki Ayra Starr amezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha video katika ukurasa wake wa TikTok akicheza wimbo mpya wa Naira Marley uitwao ‘Pxy Drip (I'm Back).
Tukio hilo halikupokelewa vyema na baadhi ya mashabiki kutokana na tuhuma zinazomkabili Naira kuhusiana na kifo cha aliyekuwa msanii wake marehemu Mohbad kilichotokea mwaka 2023.
Aidha kufuatiwa na tukio hilo kulizuka mijadala mbalimbali kama ni sahihi kwa wasanii kuunga mkono kazi za wasanii wenzao wanaokabiliwa na tuhuma nzito huku wengi wao wakitoa matusi kwa kitendo alichokifanya Ayra.
Hata hivyo baada ya video hiyo kupata ukusoaji mkubwa Ayra aliamua kuifuta katika mitandao yake ya kijamii huku Naira akimkingia kifua na kuwataka wanaomkosoa waache mara moja na badala yake matusi hayo yaelekezwe kwake.
Ikumbukwe baada ya kifo cha Mohbad, Naira Marley alikabiliwa na shutuma za unyanyasaji na vitisho dhidi ya Mohbad, hali iliyosababisha baadhi ya vituo vya redio nchini Nigeria kusitisha kucheza nyimbo zake.

Leave a Reply