Hoteli yatakiwa kutoa ushahidi kesi ya Diddy

Hoteli yatakiwa kutoa ushahidi kesi ya Diddy

Mamlaka ya shirikisho yanayomchunguza Diddy imeweka wazi kuwa huenda kuna uwezekano wa kumpatia kesi ya jinai ‘rapa’ huyo huku mamlaka hiyo ikitoa wito kwa hoteli moja iliyopo Miami kufika katika Baraza kuu la Mahakama kwa ajili ya kutoa shahidi.

Kwa mujibu wa Tmz imeeleza kuwa kulingana na hati mpya za kisheria zilizofikishwa mahakamani, waendesha mashitaka wa shirikisho kutoka Wilaya ya Kusini mwa New York wametoa wito kwa hoteli iliyopo Miami kutoa nyaraka zote na ushahidi mwingine unaomuhusu Diddy.

Diddy na aliyekuwa mpenzi wake Daphne Joy wote wametajwa katika wito huo wa mahakama, huku wito huo pia ukiitaka hoteli hiyo ambayo haijawekwa wazi jina lake kutoa rekodi na nyaraka zote zinazowahusisha Diddy, Daphne pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bad Boy Entertainment.

Rekodi hizo zinazotakiwa na Mahakama ni kuanzia kipindi cha Januari 1, 2008 hati sasa ambapo vitu vinavyohitajika ni tarehe ya kuingia na kutoka hotelini, namba za vyumba, mahitaji walioagiza, taarifa za malipo, nakala za vitambulisho vyao pamoja na huduma za chumba.

Ikumbukwe kuwa Machi mwaka huu mawakala wa Usalama wa Ndani walifanya uchunguzi kwenye nyumba za Diddy ya Miami na Los Angeles wakichunguza tuhuma zinazomkabili za kujihusisha kwenye biashara za ngono na madawa ya kulevya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags