Taasisi ya Afya nchini Marekani (NIH) imekadiria hadi kufikia mwaka 2025, zaidi ya watu milioni moja wakiwemo wanaume kuambukizwa Saratani ya Ini kila mwaka na hivyo wanahimizwa kupata chanjo mapema.
Kwa mujibu wa takwimu za (MNH) Saratani ya Ini ni ya pili kwa kushambulia watu nchini inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wagonjwa wengi huku ikichangia 8.3% ya vifo vyote vinavyotokana na Saratani Duniani.
Licha ya hayo mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka hospitali ya taifa Muhimbili (MNH), Dkt. John Rwegasha, amesema idadi hiyo inaweza kuwa zaidi kwa makundi hatarishi wakiwemo na wanaotumia madawa ya kulevya.
Leave a Reply