Hilda apokea tuzo ya Guinness baada ya kuthibitika kuvunja rekodi

Hilda apokea tuzo ya Guinness baada ya kuthibitika kuvunja rekodi

Mpishi aliejizorea umaarufu kutoka nchini Nigeria, Hilda Baci amepokea ubao wake siku chache baada ya kuthibitishwa kuwa anashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kupika muda mrefu zaidi bila msaada wa mtu mwingine.

Hilda anashikilia rekodi hiyo mpya kwa kutumia saa 93 na dakika 11, akiipiku rekodi ya awali ya masaa 87 na dakika 45 iliyowekwa na Lata Tondon wa India mwaka 2019.



Inaelezwa kuwa kuingia kwenye kitabu cha rekodi za Dunia za Guinness hakusababishi malipo ya fedha kwa mtu yeyote, kwani jukumu la Guinnes world records  ni kusherehekea mafanikio bora duniani, kuwahamasisha watu wa kawaida, kutoa burudani na taarifa.

Kwa sababu hizi, hawalipi wavunja rekodi kwa mafanikio yao au kwa kutekeleza jaribio la kuvunja rekodi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags