Hichi ndio kimefanya Diddy akamatwe na polisi

Hichi ndio kimefanya Diddy akamatwe na polisi

Ikiwa yamepita masaa machache tangu kukamatwa kwa ‘rapa’ Diddy tayari waendesha mashitaka wamefichua kilichomfanya mwanamuziki huyo kutiwa nguvuni kwa kueleza kuwa ni kutokana na kile kilichokutwa katika nyumba zake za Los Angeles na Miami.

Kwa mujibu wa TMZ mamlaka zilifichua kuwa wakati wa msako nyumbani kwa Diddy walikuta vitu kama dawa za kulevya, zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainishi na bunduki tatu za AR-15 zenye nambari za usajiri usio wake.

Mbali na hayo waendesha mwashitaka wanadai kuwa kukamatwa kwake pia kunajumuisha tuhuma za vurugu dhidi ya wanawake, kuwapiga wanawake kadhaa kwa ngumi, kuwarusha, kuwapiga mateke na kuwarushia vitu vywao.

Aidha Diddy kwa sasa anakabiliwa na mashitaka matatu ambayo ni kufanya uhalifu kwa kutumia nguvu, biashara ya ngono kwa kutumia nguvu, na kumiliki silaha isiyo na usajili wa jina lake.

Utakumbuka kuwa nyumba za Diddy zilizopo Los Angeles na Miami zilipigwa msako na mamlaka wa usalama wa Taifa kufuatia na tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizokuwa zikimkabili toka mwaka jana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags