Hersi akutana na Rais wa PSG

Hersi akutana na Rais wa PSG

Rais wa ‘klabu’ ya #YangaSC na mwenyekiti wa vilabu Barani Afrika, Eng Hersi Said amekutana na Rais wa ‘klabu’ ya Paris Saint-Germain (PSG) ya #Ufaransa na Mwenyekiti wa Vilabu Barani Ulaya, Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi, Jijini Paris nchini humo jana Jumatano.

Eng Hersi alipewa mualiko maalum kutoka kwa #Nasser kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya vilabu na wanachama.

Pia Rais huyo alimkaribisha Eng Hersi kushuhudia mchezo wa ‘Fainali’ ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa ‘Parc de Prince’, ambapo ‘klabu’ ya #PSG ilibeba Ubingwa baada ya kuichapa ‘timu’ ya Toulouse magoli 2-0.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags