Hekima za Dulla Makabila

Hekima za Dulla Makabila

Kama ilivyokawaida ya mkali wa singeli nchini, Dulla Makabila kushusha jumbe tofauti tofauti katika ukurasa wake wa Instagram huku mara nyingi ukiwa ni wa kuwapa madini mashabiki zake, hivyo basi siku ya leo hajaacha ipite bila ya kutoa neno.

Dulla kupitia Instagram yake ameshusha ujumbe wa kuwapa faida mashabiki zake kwa kuwaeleza watu kuwamakini kwenye kuchagua marafiki kwa sababu alichokigundua ni kwamba urafiki una gharama kubwa.

Kwani rafiki yako ndiyo mtu pekee anayeweza kukuumiza kuliko mtu yeyote yule, huku akitolea mfano kwa ndugu hata iweje lazima ukubali kuwa huyo ni ndugu yako maana hakuna aliyeambiwa achague ndugu wa kuzaliwa naye.
Makabila hakuishia hapo na kusema kuwa rafiki siyo kama ndugu kwa sababu rafiki ni moyo wako ndiyo umechagua kumpa dhamana licha ya kukutana na watu wengi .

Mkali huyo alimalizia kwa kuwataka watu kuwamakini na watu waliowachagua kuwa marafiki na kuhakikisha ni watu sahihi maana wakikukosea unaumia kiukweli kwa sababu ya dhamana uliyompa na imani uliyoiweka kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags