Hawa ndio wasanii walionyakuwa tuzo nyingi 2023

Hawa ndio wasanii walionyakuwa tuzo nyingi 2023

HAWA NDIYO WASANII WALIONYAKUA TUZO NYINGI MWAKA 2023


Mwaka 2023, wapo baadhi ya wasanii ambao wanatamani mwaka huu uishe ili wajaribu tena mwakani lakini wapo waliobahatika kuandika historia kwenye vitabu vyao kutokana na mafanikio waliyopata mwaka huu.

Licha ya kuwepo waliozingua na waliofanikiwa lakini unaweza sema mwaka 2023 umekuwa mwaka wa mafanikio kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, na kuwapatia maokoto baadhi ya wasanii kwa kujizolea madili ya ubalozi na kujibebea tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kwa kulitambua hilo Mwananchi Scoop imekuletea tatu bora ya wasanii alioongoza kupokea tuzo kwa mwaka 2023.

Diamondplatnumz

kwa mwaka 2023 Diamond amekamilisha jumla ya tuzo tano ambazo tatu zikiwa zinatoka nje ya Tanzania na moja ndani ya nchi. Tuzo ya kwanza aliyopata Simba la Masimba Dangote ni tuzo ya Best African Act Award kutoka MTV European Music Awards, ambayo inakuwa tuzo ya tatu sasa kwa Mondi kupokea kutoka MTV/EMA, jambo linalofanya awe msanii wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya tuzo za MTV/EMA.

Ambapo mbili aliwahi kupokea mwaka 2015 kwa usiku mmoja kama Best African Act na Best Worldwide Act (African/India).

Mbali na hiyo ya MTV mkali huyu kwa mwaka huu ameweza kuibuka kidedea na tuzo ya Best Artist East Africa, kutoka Trace award zilizofanyikia Kigali Rwanda octoba 21. Tuzo ya Best Male View’s Choice Digital kutoka Tanzania Music Awards zilizotolewa jijini Dar es salaam April 29.


Mkali hajaishia hapo akasepa tena na tuzo ya Collaboration Of The Year kutoka Tanzania Music Awards kupitia wimbo uitwao “Nitongoze” aliofanya na Rayvanny. Mwisho ni tuzo ya Best Female East Africa , kutoka Afrimma Awards zilizotolewa Dallas, texas septemba 17. Kwa ujumla inakamilisha tuzo tano za Simba kwa mwaka 2023.


Zuchu
Zuchu anaongoza gurudumu kwa wasanii wa kike kwa kujizolea tuzo nyingi mwaka 2023 ambazo zote ni kutoka Tanzania Music Awards na kuwa na jumla ya tuzo tano ambazo ni Best Bongo Fleva Song Of The Year kupitia wimbo wa Kwikwi, Best Female Artist , Best Female Bongo Fleva Of The Year, Best Music Video Of The Year kupitia wimbo wa Mwambieni, na Best Female Viewer’s Choice Digital.

Harmonize
Konde Boy 2023 pia amekuwa msanii aliyeongoza kwa kusepa na tuzo nyingi kwa mwaka huu na kupelekea jina lake kuendelea kujizolea umaarufu kwenye mataifa mbalimbali.

Mwaka huu mkali huyu wa Bongo fleva ameweza kujishindia tuzo tatu nje ya nchi na moja ndani ya nchi jumla amepata tuzo nne kwa mwaka 2023. Upande wa tuzo za African Entertainment Awards, USA (AEAUSA), zilizofanyika Marekani, NewJersey November 11, alijizolea tuzo ya Best Music Video kupitia wimbo wa ‘single again’, tuzo ya Best Artist of the Year na Afro Bongoking of East Africa.

Haikuishia hapo pia alijibebea tuzo ya Best Male Musician of the Year, kutoka Tanzania Music Awards zilizofanyika jijini Dar es salaam Aprili 29.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags